Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:46 am

NEWS: KIONGOZI WA MYANMAR AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA

Kiongozi wa Myanmar aliyeondolewa Madarakani na Jeshi la Nchi hiyo Aung San Suu Kyi amehukumiwa kifungo cha miaka nne jela.

Bi Suu Kyi alipatikana na hatia kutokana na mashitaka ya uchochezi na kuvunja maagizo ya covid 19 chini ya sheria ya majanga ya asili.

Bi Suu Kyi anakabiliwa na mashitaka 11 ambayo yanaonekana kumfunga maisha kiongozi huyo mwenye tuzo ya Heshima ya Noble.

Suu Kyi mwenye umri wa miaka 76, alikuwa ni kiongozi aliyechaguliwa na serikali ya kiraia kabla ya kung'olewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwezi Februari.

Jeshi lilinyakua mamlaka likidai kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana ambapo chama cha Suu Kyi kilipata ushindi wa kishindo.

Tangu wakati huo Bi Suu Kyi aliwekwa kwenye kifungo cha ndani na kushitakiwa mashitaka mbali mbali, yakiwemo ya ufisadi, kukiuka sheria ya siri rasmi na kuchochea ghasia za umma