- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA MYANAMAR APINDULIEWA NA JESHI
Jeshi nchini Myanamar limefanikiwa kumpindua Kiongozi wa nchi hiyo Aung San Suu Kyi mapema hii leo na sasa kiongozi huyo amewekwa chini ya ulinzi na jeshi hilo yeye pamoja na viongozi wakuu wa nchi hiyo.
Taarifa hii imetolewa na chama chake, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo iliyozua hofu ya kutokea mapinduzi.
Rais Win Myint na viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa chama tawala pia wamekamatwa mapema leo, amesema Myo Nyun msemaji wa chama hicho cha National League for Democracy.
Akizungumza kwa njia ya simu na shirika la habari la dpa, Nyun amesema wakati wowote naye anaweza kukamatwa na wanajeshi hao.
Tangu wiki iliyopita jeshi la Myanmar limekuwa likitishia kufanya mapinduzi kwa madai kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi uliopita wa mwezi Novemba uliokipa ushindi chama cha Suu Kyi cha NLD