- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KILICHOMUUA BABU WA LOLIONDO MWASAPILA HIKI HAPA
Arusha. Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Raymond leo amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mchungaji aliyejizolea umaarufu nchini Tanzania Ambilikile Mwasapila maarufu kama Babu wa Loliondo ambapo kimsingi amesema aliugua kwa siku nne mfululizo na alipokuwa anaulizwa na Wasaidizi wake juu ya anaendeleaje alikuwa anawaficha na hakuwa anataka wajue kama anaumwa.
"Alisema chembe ya moyo inamuuma sana na alipokuwa anapelekwa Hospitali alianza kutapika na hapo ndipo alipotutoka alikuwa hataki aonekane anaumwa sana na Wasaidizi wake, pale hakai na Familia tunawatafuta Watoto wake tukae vikao ili tujue atazikwa wapi" amesema DC Raymond
CHANZO CHA KIFO CHAKE.
Chanzo cha kifo cha Mchungaji Ambilikile Mwasapile (86) kimetajwa aliugua nimonia kali ambayo ilimsababisha kupata tatizo la upumuaji katika mapafu yake na homa kali.
Alipofatiki wasaidizi wake na majirani wamekuwa wakieleza kushtushwa na kifo hicho ambacho kimetokea akiwa anaendelea kutoa huduma ya tiba ya kikombe aliyoanza tangu mwaka 2011.
Mchungaji Ambilikile ambaye ataendelea kukumbukwa kwa kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2011 hadi 2013 kutokana na tiba yake ya kikombe alifariki jana saa 9:45 jioni.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala amesema kuwa taarifa za awali za madaktari zinaeleza chanzo cha kifo ni nimonia ambapo kwa takriban siku tano alikuwa anaumwa na kupata sindano za masaa.