Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:05 pm

NEWS: KIGWANGALLA AWATAKA VIONGOZI WALIOKO JUU KUFANYA MAAMUZI MAGUMU

Mbunge wa Nzega Vijijini Hamisi Kigwangalla ameishauri serikali ya Tanzania kuharakisha uvunaji wa gesi ilipo tayari kwasasa nchini.

Kigwangalla ametolea Hoja ya kwamba kama tukichelewa kuivuna tutajikuta kama taifa hatufaidiki nayo.

"Tumekuwa wagumu na waoga sana wa ‘kupigwa’ kiasi kwamba walio kwenye nafasi za kufanya maamuzi badala ya kuisaidia wanakwamisha kwa wasiwasi wa kuibiwa ama kuitwa mafisadi. Mambo hayaendi. Msumbiji ambao ni jirani zetu wanasonga mbele, sisi tumekwama" amesema Kigwangalla leo Bungeni.

Amesema kuwa Wawekezaji wanakimbilia huko(Msumbiji) wenzetu wanafaidika. Nimefanya utafiti na kubaini kwamba, ili tusonge mbele tunahitaji kubadili mtazamo wetu, tubadili staili yetu ya ku-negotiate - tukubali tu kuwa hatuna uwezo wa kutosha ku-negotiate mikataba hii mikubwa na ya kimataifa, hivyo tuajiri ‘transaction advisor’ atusaidie tukamilishe majadiliano na wawekezaji wa kwenye sekta ya gesi"