- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIFUSI CHAUWA WATATU KIGAMBONI DAR
Dar es salaam. Watu watatu wote wenye jinsia ya Kiume wamefariki dunia na Wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya mara baada ya kufukiwa na kifusi cha kokoto wakati wakiwa kwenye shughuli za machimbo ya mawe katika eneo la machimbo ya Kikikaka, Mji Mwema Kigamboni, Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na miili mitatu ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni na majeruhi mmoja amepatiwa matibabu na kuruhusiwa "Waliofariki ni Ally Fundi (18), Mohamedi Maganga (26) na Kashinde Msigale"
Nyangasa amesema "Machimbo haya yalishafungwa tangu mwaka 2018 lakini Watu walikuwa wanakuja kuchimba kwa kuibiaibia tu, niwakumbushe tena Wananchi bado maeneo haya yamefungwa hayaruhusiwi kuchimba na tutaweka ulinzi ili kuzuia Watu wasije"
"Wananchi wa eneo hili atakayekuwa na taarifa ya kutomuona Ndugu yake anayefanya shughuli zake hapa atuambie tuendelee na shughuli za ufuatiliaji, sio kwamba tumemaliza leo tutaendelea kufuatilia"