Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:01 pm

NEWS: KESI YA SABAYA YASHINDWA KUENDELEA

Muakilishi Publisher Julai 2, 2021

Arusha. Kesi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake watano wanaokabiliwa na mashtaka sita yakiwemo mawili ya ujambazi wa kutumia silaha imeahirishwa hadi Julai 16, mwaka huu.

Leo Ijumaa Juni 2, 2021 ndio ilikuwa siku ya mashahidi upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao lakini ikaelezwa na wakili wa Serekali kuwa hawapo.

Wakali wa Serekali Tarsila Garvas ameileza mahakama kuwa mashtaka mengine manne kati ya yale 6 yanayowakabili watuhumiwa hao upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili Garvas aliiomba Mahakama kupangwa siku nyingine ili mashahidi hao waanze kutoa ushahidi wao na hakimu mkazi mkuu, Salome Mshasha alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 16, 2021.

Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Sabaya na wenzake wawili walisomewa mashtaka mawili.

Siku hiyo ilielezwa kuwa Februari 9, 2021 katika mtaa wa Bondeni, Sabaya akiwa na watuhumiwa wenzake wawili walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kuvamia duka la Said Saad na kuwaweka chini ya ulinzi.

Ilielezwa kuwa Sabaya na walinzi wake, Sylivester Nyingu (26) maarufu Kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa hilo baada kumfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetini na kumuibia 390,000.

Katika tukio hilo wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao pia wanatuhumiwa kumpiga mateke kumtishia silaha na kumpora simu na Sh35,000 Ramadhani Ayoub. Watuhumiwa hao ambao walikana mashtaka yanayowakabili wanatetea na wakili, Moses Mahuna.

Leo kabla ya kuanza kwa kesi hiyo ulinzi uliimarishwa vyakutosha na kulikuwa na idadi ndogo kiasi ya watu walifurika Mahakamani ukilinganisha na siku ya kwanza alivyofikishwa mahakamani. Wengi wao wakitaka kuendelea kushuhudia na kufuatilia mwendendo wa kesi hiyo maarufu mkoani kilimanjaro.

Muakilishi Publisher Julai 2, 2021