- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAULI YA HALIMA MDEE BAADA YA KUAPISHWA
Dar es Salaam. Mbunge mpya wa Viti Maalum Chadema, Halima Mdee amesema kuwa nafasi ya viti maalum waliopata sio hisani bali ni sehemu ya ushindi walioupata chama chao kupitia Mgombea Urais wa chama hicho Tundu Lissu kwenye uchaguzi Mkuu uliopita.
Mdee amewaahidi wanachama wa chama hicho kuwa wanakwenda bungeni kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu.
Akizungumza katika viwanja vya Bunge leo Jumanne Novemba 24, 2020 muda mfupi baada ya kula kiapo pamoja na wabunge wenzake 18, Halima ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) amesema, “nikushukuru kwa kiapo kufanyika na kukamilika, nikishukuru chama changu kupitia wao sisi tumepata nafasi hii ya kukiwakilisha chama chetu. Viti hivi sio hisani ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.”
“Nikuhakikishie mheshimiwa spika tutafanya kazi kwa uaminifu kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile tulivyokuwa tunavifanya. Kuna vijana wapya sisi kama dada zao tunakuhakikishia watafanya kazi bora. Niwahakikishie wana Chadema tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na uadilifu mkubwa sana.”
Amesema, “kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya nchi chama chetu kimekidhi kigezo vya kupata viti maalumu, viti hivi si hisani ila ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kimepata.”
Wakati huo huo katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika amesema kuwa wao kama chama hawajatuma Orodha ya majina ya viti maaluk kwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ili yapelekwe ofisi ya Bunge.
Mnyika amesema kinachofanyika sasa ni uhuni na wanafuatilia kwa karibu ili wachukua hatua dhidi ya hujuma hizo.