Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:13 pm

NEWS: KATAMBI AWATAKA WANANCHI WASILALAMIKIE MAKATO YA SIM

Shinyanga. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira Patrobas Katambi, amewataka wananchi wasilalamike juu ya makato ya miamala ya simu na ongezeko la bei ya mafuta kwa kuwa serikali ina nia nzuri ya kuwaletea maendeleo.

Katambi ambaye pia ni MBUNGE wa Shinyanga Mjini amebainisha hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mnada wa Oldshinyanga, wakati akila nao nyama choma.

Amesema makampuni ya simu yameingia kwenye mfumo wa kibenki, hivyo serikali imeona ni njia nzuri ya ukusanyaji kodi kupitia makato ya miamala ya simu, ili ipate fedha za kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Ndugu zangu kupitia makato hayo ya miamala ya simu, kiasi cha fedha kitakacho patikana, ambapo shilingi bilioni 45 zitatengwa kujenga maboma 900, zahanati 500, vituo vya afya 114, maboma 2,500 shule za sekondari, na madarasa 10,000 kwa nchi nzima”

"Pia kwa upande wa mafuta zinatengwa shilingi milioni 500 kujenga barabara za ndani nchi nzima , na haya ni machache tu ambayo nimeyasema kuna mambo mengi ambayo yatatekelezwa chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassani," amesema Katambi.