Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 1:51 pm

NEWS: Kampuni ya TTCL yazindua teknolojia mpya ya 4.5 G nchini

Dar es salaam: TTCL- kwa kushirikiana na Kampuni ya kimataifa ya Huawei imezindua teknolojia ya mtandao ya 4.5G ambayo itasaidia TTCL kutoa huduma kwa ufanisi nchi nzima.

Uzinduzi ukifanyika. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G

Akizindua mtandao huo jijini Dar Es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano Profesa FAUSTINE KAMUZORA amesema teknolojia hiyo itawawezesha watanzania wengi hasa waliopo vijijini kupata mawasiliano ya uhakika ya simu.