- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JUKWAA LAIBANA SERIKALI MIRADI YA KILIMO.
DODOMA: Jukwaa la Wanawake Wakulima Wadogo Tanzania (JUWAWATA) wameiomba Serikali kuifufua miradi mikubwa ya Kilimo ambayo ilikuwa na tija lakini imekwama kwa muda mrefu.
Zaidi ya miradi 61 yenye thamani ya mabilioni ya fedha imetekelezwa na mingine kutofanyiwa ukarabati hivyo kuwakosesha fursa wakulima.
Akizungumza katika mkutano na Wakurugenzi wa Wizara ya Kilimo, Rais wa Jukwaa la Wakulima Wanawake Tanzania Amina Senge, alisema miradi hiyo ilikuwa mkombozi mkubwa kwa wanawake lakini haifanyi kazi na mingi imebadilishiwa matumizi.
Mkutano uliitishwa na Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid kwa lengo la kufanya tathimini ya miradi iliyokufa na ambayo haifanyi kazi ili kuomba ifufuliwe.
Senge alisema wakulima wamekuwa wakilalamikia kuhusu miradi hiyo kwa muda mrefu lakini wameshindwa kupata ufumbuzi.
Baadhi ya miradi aliyoitaja Senge ni ekari 560 za mradi wa umwagiliaji Kata ya Itilima ambao uligharimu Sh302.13 milioni 2005 lakini ulifanya kazi msimu mmoja tu.
Mingine ni mradi wa umwagiliaji wa bustani uligharimu Sh298 milioni katika kijiji cha Nyenze lakini kwa miaka 9 haufanyi kazi huku majengo ya miradi ya Kilimo wilaya ya Chamwino mingi yamegeuzwa Ofisi za Watendaji.
"Majengo ya benki ya mazao, zimekuwa kumbi za starehe, Viwanda vinajengwa lakini TBS hawatoi vibali na baadhi ya vituo vimekuwa maghara ya kuhifadhia vifaa vya Tasaf, tunaomba Wizara iangalie hatma ya wakulima," alisema Senge.
Wakulima hao walipendekeza Wizara ya Kilimo kuangalia uwezekano wa kuifufua baadhi ya miradi hiyo japo kwa awamu ili kuwarudishia wakulima matumaini.
Amina Dafi alisema miradi iliyokwama ni mingi lakini wameichukua kwa uchache kama mfano lakini akasema kama ingefufuliwa yote ingekuwa sehemu ya ukombozi kwa wakulima.
Dafi alisema sehemu kubwa ya miradi hiyo ni kama imesahaulika kwani Serikali haionyeshi namna gani inaijali miradi hiyo ndiyo maana majengo yanatumika kwa shughuli zingine bila kujali.
Ofisa bajeti na mipango wa Wizara ya Kilimo Timotheo Semuguruka alisema Serikali iko mbioni kuifufua miradi hiyo kwani faida yake ni kubwa kuliko ilivyo sasa.
Semuguruka alisema wanapoelekea kwenye bajeti, baadhi ya miradi wataingiza kwenye bajeti zao ili waanze kuifufua kwani inati aibu inapoachwa wakati mingine inatokana na fedha za wafadhiri na wadau.