- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JOE BIDEN ATEUA WAFANYAKAZI WANAWAKE IKULU
Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameweka historia katika ikulu ya Marekani mara baada ya kuchagua wafanyakazi wote wa habari waandamizi katika Ikulu hiyo kuwa wanawake.
Jopo hilo litaongozwa na Mkurugenzi Kate Bedingfield, aliyekuwa naibu mkurugenzi wa mawasiliano wakati wa kampeni yake.
Jen Psaki, ambaye alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Rais Barack Obama Ikulu, atakuwa waziri wa habari.
Bwana Biden ameahidi kuwa na utawala wake unaojumuisha kila mmoja Marekani.
"Ninafuraha kuwatangazia leo, timu ya mawasiliano Ikulu inajumuisha wanawake tu," Bwana Biden amesema katika taarifa.
"Timu hii ya wanawake waliohitimu wenye uzeofu, inajumuisha kila moja na imejitolea kwa pamoja kujenga tena nchi hii."
Watakao msaidia makamu rais Kamala Harris katika masuala ya habari na mawasiliano watakuwa ni Symone Sanders na Ashley Etienne.
Tofauti na nafasi zingine katika baraza la mawaziri, ofisi hii ya habari na mawasiliano haihitaji kuthibitishwa na bunge la Seneti.
Bwana Biden ataapishwa kuchukuwa rasmi majukumu ya rais Januari 20.