Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:38 am

NEWS: JESHI LAWARUDISHA KAMBINI VIJANA WA JKT WALIORUDISHWA NYUMBANI

Dodoma. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana wote waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 kuripoti katika makambi yao waliyopangiwa hapo awali kati ya Mei 7 hadi 14, 2021, huku ikielezwa kuwa utaratibu huo hautawahusu wenye elimu ya kidato cha sita, cheti, stashahada, shahada na taaluma ya uhandisi.

Jeshi liliwarejesha vijana hao wa JKT Mnamo Februari, 2021 na kuwarejesha vijana hao nyumbani kwao bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Aprili 30, 2021 na mkuu wa JKT, Meja Jenerali Charles Mbuge ikielezwa kuwa wanaotakiwa kuripoti ni wale wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne.

Akizungumzia uamuzi huo, kaimu mkuu wa utawala wa JKT, Kanali Hassan Mabena amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa awali na kubainisha kuwa wanaotakiwa kuripoti ni wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne.

“Vijana wenye elimu ya kidato cha sita ngazi ya cheti, stashahada, shahada na wenye taaluma ya uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa,” amesema.