November 22, 2024, 9:31 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 17
Mahakama ya Wilaya ya Njombe imemuhukumu Bright Dismas (25) Mkazi wa Kitisi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya makosa mawili likiwemo la ubakaji na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Isack Mlowe, ambapo amesema tukio hilo la ubakaji lilitokea mwaka jana mwezi February.
"Mshtakiwa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na Mwanafunzi huyo ambapo siku ya tukio alikwenda nyumbani kwao akiwa peke yake, aliingia ndani na kuandaliwa chakula na Mwanafunzi huyo kisha baadaye wote wakaenda chumbani na kufanya mapenzi"