- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAJI MKUU AWATAKA MAJAJI NA MAHAKIMU KUSOMA SHERIA ZA UCHAGUZI ILI KUTENDA HAKI
JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amewataka Majaji na Mahakimu wote nchini kusoma sheria na kanuni zote zinazohusu Uchaguzi Mkuu, ili kutoa maamuzi ya mashauri ya uchaguzi kwa weledi na kutenda haki.
Jaji Prof. Juma, aliyasema hayo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya namna bora ya uendeshaiji wa mashauri ya uchaguzi kwa maafisa wa Mahakama wapatao 282.
Alisema kuwa, Majaji pamoja na wote watako pata nafasi ya kusikiliza mashauri ya uchaguzi mkuu 2020, wanatakiwa kuwa na uelewa mpana juu ya sheria pamoja na kanuni zitakazo tumika ili kutenda haki.
Pia, alisema maafisa wote wa Mahakama ambao watapata nafasi ya kuskiliza mashauri ya uchaguzi mwaka huu, wanatakiwa kutumia muda wao hivi sasa kuzisoma sheria pamoja na kanuni ili kujiongezea uelewa.
“Tunatakiwa kutenda haki kwa mashauri yote yatakayoletwa kwetu na kuyafanyia kazi ili kutoa maamuzi kwa weledi na kuzingatia haki kwa wale watakao onewa katika mchakato wa uchaguzi mkuu mwaka huu”alisema Jaji Prof. Juma
Alieleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maofisa wa mahakama kutoa maamuzi kwa weledi na haki kwa wakati.
“Mahakama isionekane kupendelea upande fulani wa uchaguzi, bali Mahakama iisaidie Tume ya taiafa ya uchaguzi NEC, kuwapatia wananchi uchaguzi huru na wa haki, pia Majaji wajikite katika kusoma vifungu ambavyo vitawasaidia kutoa maamuzi yote ya mashauri ya uchaguzi kwa wakati”alieleza.
Vile vile, aliwataka maafisa wa Mahakama kushughulikia mashauri ya jinai wakati wa kamapeni, katika uchagumzi mkuu 2020.
“Makosa ya jinai ambayo mnatakiwa kuyashugulikia ni yale ya wakati wa kampeni pamoja na wakati wa kupiga kura makosa hayo ni kama vile kujiandikisha maeneo zaidi ya moja, kupiga kura katika kituo zaidi ya kimoja, kudanganya kitambulisho na mengine mengi.”Alibainisha