- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAJI MKUU AIOMBA SEREKALI KUONGEZA MAGEREZA
Iringa. Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ameiomba Serikali kutanua wigo kwa kuongeza ujenzi wa magereza kwa kila wilaya nchini ili kupunguza msongamano wa mahabusu na ucheleweshaji wa kesi.
Jaji Juma ametoa ombi hilo mjini Iringa leo Agosti 9 alipokuwa akifungua mkutano baina ya Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania na Kamati ya maadili ya mkoa wa Iringa na wilaya zake tatu za Iringa, Kilolo na Mufindi uliofanyika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa.
Prof. Juma amesema msongamano katika mahabusu unatokana na kukosekana kwa mahabusu katika mahakama za wilaya na hivyo kusababisha watuhumiwa kusafirishwa umbali mrefu na wengine kesi zao kusikilizwa kwa muda mrefu.
"Mnapokwenda kujenga mahakama, Serikali ijenge magereza katika wilaya zilizopo mahakama. Hii itasaidia kupunguza msongamano wa mahabusu na ucheleweshwaji wa kesi kutokana na miundombinu hiyo kwani hupelekea hakimu mmoja kushughulika na kesi za wilayani na za mikoani," alisema Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu alisema katika baadhi ya maeneo yasio na magereza watuhumiwa wa kesi mbalimbali wamekuwa wakipelekwa katika magereza mengine ya nje ya wilaya jambo linaloathiri mahudhurio yao mahakamani.
Amesema Mahakama inatekeleza mpango wake wa miaka mitano unaolenga kupunguza changamoto za miundombinu ya mahakama na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ili kurahisisha huduma ya utoaji haki.
Kwa kupitia mpango huo alisema Mahakama inakusudia kujenga mahakama 25 katika wilaya zisizo na huduma hiyo.