- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AAGIZA KUKAMATWA KWA MGURUGENZI ALIYEAGIZA BIDHAA ZILIZOHARIBIKA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira)Selemani Jafo ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mkurugenzi wa Kampuni ya Seif for Tobacco Trading Co. Ltd Bw. Kaissy aliyeingiza nchini makontena zaidi ya 500 yenye malighafi ya Molasesi iliyoharibika nakuyatelekeza Bandari ya Dar es salaam.
Waziri Jafo ameagiza hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia makontena hayo yakiwa yametelekezwa bandarini hapo na mengine kutawanywa katika baadhi ya bandari kavu jijini Dar es Salaam.
Waziri Jafo ameagizwa kukamatwa mara moja mfanyabiashara huyo aliefahamika kwa jina moja tu la Kaissy, kufuatia ziara ya kushtukiza bandarini hapo, hii leo Mei 3, 2021.
Aidha Waziri Jafo pia ametembelea bomba la kusafirishia mafuta kutoka kwenye meli na kubaini uvujaji wa mafuta katika mabomba hayo unaosabishwa na uchakavu wa mitambo hiyo, Waziri Jafo ameagiza hatua za haraka kuchukuliwa kudhibiti uchafuzi wa Mazingira.