- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IRAN YAWAKAMATA MAMLUKI WA KIJASUSI WA ISRAEL
Mamlaka za kijasusi nchini Iran zimewakamata watu wanne akiwemo kiongozi wa matandao wa kijasusi wanaohusishwa na vitengo vya kijasusi vya Israel (MOSSAD).
Iran haijataja uraia wa majasusi hao japokuwa inasema kuwa watu hao walikuwa wamepokea mafunzo ya kuendeleza oparesheni za kijeshi na kuhujumu nchi hiyo.
ofisi ya waziri mkuu nchini Israeli inayosimamia majasusi wake walioko nje ya nchi Mossad, imekataa katu katu kuzungumzia madai ya Iran kuwa inawashikilia maafisa wao.
Iran na Israel hazijakuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu, mataifa hayo yakikabiliwa na mvutano kuhusu mpango wa nyukilia wa Iran.
Israel imekuwa ikiituhumu Iran kwa kuyauunga mkono makundi ya waasi dhidi yake, Iran nayo ikiituhumu Israeli kwa kuwauua baadhi ya maofisa wake yakiwemo mauwaji ya afisa wa ngazi ya juu wa Iran mwezi Mei. Madai ambayo Israeli haijakana wala kukubali.
Wiki iliyopita maofisa wa usalama nchini Iran walisema kuwa waliwakamata watu waliodaiwa kuwa wanaifanyia kazi Israeli ambayo waliingia nchini humo kutokea Iraq wakiwa na nia ya kutekeleza oparesheni za kigaidi.
Haya yanajiri wakati huu ambapo uhasama kati ya Iran na Israeli ukiendelea kuongezeka, Israeli ikiaapa kutumia njia zote zilizopo kuizuia Iran kuendeleza mpango wake wa kujenga kinu cha nyukilia.
Wachambuzi wa mambo wanahisi kuwa uhasama kati ya Iran na Israeli huenda ukaongezeka zaidi hivi karibuni kwa kuwa tayari Urusi imejipenyeza moja kwa moja kuwa mshirika wa karibu wa Iran.