- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: INJINIA MFUGALE AFARIKI DUNIA DODOMA
Dodoma. Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS Mhandisi Patrick Aron Nipilima Mfugale amefariki Dunia hii leo Katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Taarifa zinadai kuwa Mfugale jana mchana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu wa ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi.
Baada ya kufika Dodoma usiku wa jana alianza kujisikia vibaya. leo saa tano asubuhi alizidiwa na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.
JE MFUGALE NI NANI ?
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja alioweza kujenga ni:
- Daraja la Mkapa Rufiji
- Mfugale Dar es salaam.
- Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na
- Mozambique huko Ruvuma.
- Daraja la Rusumo huko Mara
- Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
- Daraja la Nyerere huko Kigamboni
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
- Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
- Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.