Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:14 pm

NEWS: IDRISS SULTAN ABADILISHIWA MASHTAKA

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idrisa Sultan na wenzake wamefutiwa mashtaka yao ya hapo awali ya kurusha maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufunguliwa mashtaka mapya kwa hakimu mwingine.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka upya jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Luboroga

Mbali ya Idrisa, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Doctor Ulimwengu na Isihaka Mwinyimvua, ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 8 mwaka 2016 na 12, mwaka 2020 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali Adolf Ulaya alidai washtakiwa hao, walirusha maudhui online tv kwenye akaunti ijulikanayo Loko Motion bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na kesi iliahirishwa hadi Agosti 11 mwaka huu kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Awali, kesi hiyo ilifutwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi na upande wa Jamhuri ukadai kesi hiyo ililetwa kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali lakini bado hayajakamilika hivyo waliiomba mahakama ipange tarehe nyingine.

Baada ya kudai hayo Hakimu Shahidi aliamua kuifuta chini ya akifungu namba 225 cha sheria ya makosa ya jinai.

Walipoachiwa washtakiwa hao walikamatwa tena na askali waliokuwa mahakamani hapo na kuwekwa chini ya ulinzi.