- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDRIS SULTANI AACHILIWA HURU NA MAHAKAMA
Dar es salaam. Msanii wa Vichekesho nchini, Idris Sultani ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam yeye pamoja na mwezake Innocent Maiga mara baada ya upande wa Serekali kushindwa kuleta Mashahidi zaidi ya mara mbili, huku ukitoa sababu zisizo na mashiko.
Uamuzi huo wa kuwaachia huru umetolewa leo Mei 17, 2021 saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu.
Sultan alikuwa akikabiliwa na tuhuma ya kushindwa kusajili laini ya simu inayomilikiwa na mtu mwingine na mwenzake Innocent Maiga anashtakiwa kwa kushindwa kutoa taarifa.
Wakili wa Serikali Silvia Mitanto alidai kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini hawana shahidi sababu siku ya tarehe ya kesi Mei 14 ilikuwa sikukuu ya Eid.
Wakili wa utetezi, Jebra Kambole amepinga hoja hiyo kwa madai kwamba haina msingi, shauri la muda mrefu hivyo aliomba wateja wake waachiwe huru.
Baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Chaungu alisema sababu ya upande wa Jamhuri haina msingi na kwamba Februari 22 mwaka huu alitoa ahirisho la mwisho, tangu hapo hakuna shahidi hadi Aprili 29 mwaka huu ambapo pia hawakuwa na shahidi.
"Kwa mazingira hayo mahakama inalifuta shauri hili chini ya kifungu cha sheria namba 225 , washtakiwa wanaachiwa huru," alimesema na kuwaachia huru washtakiwa.
Hata hivyo washtakiwa hao bado wako chini ya ulinzi wa Polisi wakisuri maelekezo mengine kama yatakuwepo.
Maiga anakabiliwa na kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya laini ya simu kwa mtoa leseni kosa analodaiwa kulitenda kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 katika eneo la Mbezi beach Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.