- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDRIS SULTAN KUFIKISHWA MAHAKAMA KESHO
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan anakusudiwa kupandishwa kizimbani kesho kujibu shtaka lake linalomkabili la kumnyanyansa/kumuonea Rais Magufuli.
Wakili wa Mshekeshaji huyo Benedict Ishabakaki amesema mteja wake hajafikishwa mahakamani leo kama ilivyotegemewa lakani ofisi ya DCI imemuhakikishia kuwa Idris watamfikisha mahakani kesho.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wake amesema Idris wanamtuhumu kwa kuvunja kifungu cha 23 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kinachokataza uonevu wa kimtandao. Kosa hio kwa kingereza linatambulika kama 'cyber bullying'.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu akikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo anaweza kuadhibiwa faini ya Shilingi milioni tano za kitanzania au kifungo cha miaka mitatu au akapewa adhabu zote mbili.