- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDRIS SULTAN AFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUACHIWA KWA DHAMANA
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan hatimaye amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kuachiwa kwa dhamana hii leo baada yakusomewa mashtaka ya kutum namba ya simu ambayo haijasajiliwa jina lake.
Kama utakumbuka Mshindi huyo wa Big brother Africa alikamatwa siku ya Jumanne Mei 19, 2020 baada ya kujisalimisha kituo cha polisi cha Oystabey jiji Dar es Salaam.
Anayetajwa kusajili laini hiyo, Innocent Maiga pia ameshatkiwa pamoja na Bw Sultan kwa kosa la kutoarifu mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake.
Msanii huyo ameachiwa kwa dhamana baada ya watu wawili kusaini bondi ya Shilingi za Tanzania milioni 15 kila mmoja, wakili wake Bennedict Ishabakaki ameieleza BBC.
Wawili hao wanatuhumiwa kufanya makossa hayo kinyume cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektoniki na Posta, na endapo watakutwa na hatia watakabiliana na adhabu ya faini isiyopungua Shilingi milioni tano, ama kifungo kisichopungua miezi 12 ama vyote faini na kifungo.
Kesi dhidi ya msanii huyo imeahirishwa mpaka Juni 9.
Kabla ya kufikishwa mahakamani, polisi na wakili wa msanii huyo alisema kuwa Idris alikuwa pia akihojiwa kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimtandao.
Wakili Ishabakaki pia alisema alikamatwa na kuhojiwa na polisi juu ya mkanda wa video uliosambaa mitandaoni hivi karibuni akionekana akiicheka picha ya zamani ya rais Magufuli.