- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWANIA URAIS ZANZABAR
Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama cha Mapinduzi CCM kimempitisha Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Dkt Hussein Mwinyi kugombea nafasi ya urais katika Visiwa vya Zanzibar.
Dkt Mwinyi ni Mbunge wa jimbo la Kwahani, Zanzibar na Waziri wa Ulinzi katika serikali ya muungano. Huyu ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya pili ya serikali ya Jamhuri ya Mungaano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Kabla ya Dr. Mwinyi kutangazwa Mshindi, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM alisema “Wote hawa watatu ambao tutawapigia kura ili kumpata mmoja wanafaa ila yupo mmoja anayefaa zaidi ni jukumu lenu kumchagua anayefaa na nina matumaini kati ya hawa mmoja atakuwa Rais wa Zanzibar”
“Tusichukiane, mimi niliomba kura na Mzee Pinda na nikampindua, Makongoro Nyerere na wengine ila leo tupo hapa,kazi hizi ni za kupita, wagombea wote 31 nawapongeza kwa kuchukua fomu atakayepita mmoja tumuunge mkono, saa nyingine maneno yanaletwa na upinzani na CCM tunayabeba”- Rais Magufuli.
Jina la Mwinyi sasa litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ili kumthibitisha rasmi kuwa mgombea wa CCM Zanzibar.
Dkt Mwinyi amepitishwa kwa kura 129 sawa na asilimia 78 ya kura zote.
Mwinyi alikuwa akikabiliana na upinzani kutoka kwa wanachama wenzake akiwemo Shamsi Vua Nahodha aliyepata kura 16 na Dkt Khalid Salim Mohammed aliyepata kura 19.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura hizo Mwinyi aliwashukuru wajumbe wote kwa kuonesha imani kwake.
"Hizi ni kura nyingi sana...nikuahidini kuwa tutakuwa pamoja tukatafute ushindi wa Chama Cha Mapinduzi,"
Yuko katika shughuli za kisiasa tangu mwaka 2000, hapa ni kusema sio mgeni katika uwanda wa siasa za Tanzania.
Ametumikia nafasi ya ubunge pande zote za Muungano, alikuwa Mbunge katika jimbo la Mkuranga, mkoa wa Pwani kabla ya kuwa Mbunge wa Kwahani.