Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 4:27 pm

NEWS: HUMAN RIGHTS WATCH YAITAKA SADC KULAANI KINACHOFANYWA NA ZIMBABWE

Zimbabwe's 'New Dispensation' destroys hope on human rights | Africa at LSE

Shirika linalojihusisha na kutetea haki za binadamu la Duniani la Human Rights Watch limezitaka nchi zote za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, kukemea vikali hadharani ukandamizaji uliofanywa na serikali ya Zimbabwe dhidi ya maandamano ya amani ya kupinga ufisadi yaliyofanyika Julai 31.

Shirika hilo pia limelaani kamata kamata ya kiholela dhidi ya wapinzani nchini humo.

Zimbabwe police use force to disperse opposition crowd | Zimbabwe News | Al Jazeera

Katika ripoti yake iliyochapishwa Hii leo, Human Rights Watch inasema kuwa serikali ya Zimbabwe imewakamata kuhusiana na maandamanano hayo, watu wasiopungua 60, miongoni mwao akiwemo mwandishi wa vitabu Tsitsi Dangarembga na msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change, MDC Fadzayi Mahere.

Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika ukanda wa kusini mwa Afrika Dewa Mavhinga amesema SADC na Umoja wa Afrika, AU zinapaswa kuikemea serikali ya Zimbabwe kwa ukandamizaji huo na vitendo vingine vya uvunjifu wa haki za binadamu vinavyofanyika katika maeneo yote ya nchi, na kuueleza bayana uongozi wa rais Emmerson Mnangagwa kuwa vitendo hivyo vinakwenda kinyume na mikataba ya Umoja wa Afrika kuhusu haki za binadamu, na kwamba hilo halikubaliki.

Watu 16 walipatata majeraha yaliyowalazimu kutibiwa hospitalini, imeongeza ripoti hiyo. Dangarembga aliachiwa kwa dhamana siku moja baadaye.

Mkurugenzi huyo ameisifu Afrika Kusini kwa kujitokeza na kuelezea wasiwasi wake, akisema ingawa sio ncho zote za SADC zenye ujasiri wa kufanya hivyo, hilo pekee lina umuhimu wake.

''Inatia moyo kuona Afrika Kusini ikielezea wasiwasi wake, na kujihusisha na kampeni ya mtandani wa 'maisha ya Wazimbabwe yana thamani'. Hata kama hatuisikii kila nchi ya SADC ikiikemea hali nchini Zimbabwe, sauti ya Afrika Kusini kama taifa kubwa, inatosha.'' amesema Mavhinga.