Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:35 am

NEWS: HUKUMU KESI YA MEMBE NA MUSIBA YAGONGA MWAMBA

Dar es salaam. Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imehairisha Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba anayejitabulisha kama mwanaharakati huru imepigwa kalenda hii leo hadi Oktoba 28, mwaka huu.

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya jumla ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo Jumanne Oktoba 12, 2021 na Jaji Joaquine De Mello imeahirishwa kwa sababu haijakamilika kuandikwa.

Musiba katika kesi hiyo anashtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamuhujumi Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea Wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi aliyofanya kugombea Urais mwaka 2020 kupitia CCM