Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:01 am

NEWS: HILI NDILO BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Leo Desemba 5, 2020 Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri lililosheheni Wasomi mbali mbali, huku Vigogo wengi waliokuwepo hapo awali kwenye baraza la mawaziri lililopita wakikosa nafasi kwenye baraza hilo jipya.

Hii ndio orodha ya baraza jipya la mawaziri.

1.Wizara ya Maji -Aliyeteuliwa Juma Aweso

2.Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo- Aliyeteuliwa Innocent Bashungwa

3.Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu- Aliyeteuliwa Jenister Mhagama.

4.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto- Aliyeteuliwa Doroth Gwajima (Mbunge mpya alikuwa naibu katibu mkuu)

5.Wizara ya Uwekezaji ofisi ya Rais- Aliyeteuliwa Mkumbo Kitila

6.Wizara ya Katiba na Sheria- Aliyeteuliwa Mwigulu Nchemba.

7.Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia- Aliyeteuliwa Prof Joyce Ndalichako.

8.Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Aliyeteuliwa Mashimba Mashauri Ndaki.

9.Wizara ya Maliasili na Utalii- Aliyeteuliwa DK Ndumbalo Damas.

10.Wizara ya Ofisi ya Rais- TAMISEMI Suleiman Jaffo

11.Wizara ya Madini- Aliyeteuliwa Dotto Biteko

12.Wizara ya Nishati- Aliyeteuliwa Dkt Medard Kalemani.

13.Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Aliyeteuliwa (mbunge mpya), Mhandisi Dkt Leonard Chamuliho (alikuwa Katibu Mkuu Uchukuzi).

14.Wizara ya Kilimo- Aliyeteuliwa Prof.Adolph Mkenda.

15.Wizara ya Viwanda na Biashara- Aliyeteuliwa Mwambie Geofrey Idelphonce.

16.Wizara ya Mambo Ya Ndani- Aliteuliwa George Simbachawene.

17.Wizara ya Muungano na Mazingira- Ummy Mwalimu.

18.Wizara ya (Wizara mpya) ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Aliyeteuliwa Dkt Faustine Ndugulile.

19.Wizara ya Fedha- Aliyeteuliwa Dkt Philip Mpango.

20. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki- Aliyeteuliwa Prof Paramagamba Kabudi.

21 Wizara ya Ardhi- Aliteuliwa William Lukuvi

22.Wizara ya Ulinzi na JKT- Aliyeteuliwa Elias John Kuandikwa.

23.Wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora- Aliyeteuliwa Capt Mstaafu George Mkuchika.