- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAYA NDIO MATAJI YA SIMBA BAADA YA TAJI LA JANA
Klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam jana ilifanikiwa kuchukua Taji la 21 kwenye historia ya Soka Ligu kuu Tanzania Bara.
Simba wamefanikiwa kutetea taji hilo baada ya kutoka sare ya bila mabao (0-0) dhidi ya wenyeji, wao Tanzania Prisons katika mchezo uliofanyika Dimba la Sokoine.
Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2017/2018 , 2018/2019 , 2019/2020.
Sababu kubwa ya Club hiyo kufanikiwa kuchukua Ubingwa mara tatu mfululizo inatajwa kuwa ni baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya kimfumo na kimuundo ndani ya Simba.
Mabadiliko hayo ya Kimfumo yalipelekea kupata Simba Sport Company na Simba Sport Club.
Wekundu hao wa Msimbazi Simba ambao wananolewa na kocha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck wamefikisha pointi 79 baada ya sare ya leo katika michezo 32 ikijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu, kwani hakuna timu inayoweza tena kufikia alama hizo.
Hii ndio Histori ya mataji ya Simba 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012, 2018, 2019 na 2020.
Licha ya taji hilo bado Simba itakuwa na mlima mrefu kama wanahitaji kuwafikia watani wao kwenye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwani Yanga tayari wanamataji 27 baada ya kushinda miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.