Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 8:10 pm

NEWS: HATIMAYE CHAMA CHA JUBILEE CHATANGAZA KUMUUNGA MKONO ODINGA

NAIROBI. Chama tawala nchini Kenya, Jubilee kimetangaza kumunga mkono mpinzani wake Raila Odinga, kiongozi mkongo wa upinzani katika juhudi zake za kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi mkuu wa Ogusti mwaka huu.

Rais wa Nchi hiyo Uhuru Kenyatta amepongeza uwamuzi wa chama tawala cha Jubilee kumunga mkono mpinzani wake wa zamani Raila Odinga wa chama cha upinzani cha ODM kugombania kiti cha rais.

Uwamuzi huo muhimu unamuondoa Naibu Rais Wlliam Ruto kua mgombea wa chama hicho licha ya kwamba ametangaza anagombania kiti cha rais.

Mkutano wa Wajumbe wa Taifa wa chama cha Jubilee, NDC, ulofanyika mjini Nairobi siku ya Jumamosi kilitangaza pia mabadiliko kwenye uwongozi wake, kwa kumuondosha Ruto kama naibu mwenyekiti.

Nafasi ya Ruto inachukuliwa hivi sasa na Jimmy Angwenyi, na katibu mkuu wa chama Raphael Tuju anaondoka na nafasi yake inachukuliwa na Jeremiah Kioni, mbunge wa Ndaragwa.

Odinga mwenye umri wa miaka 77, aligombania nafasi ya kiti cha rais mara nne akiwa mgombea kutoka nje ya serikali, akiahidi kuleta mabadiliko lakini hakufanikiwa kupata ushindi.