- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALMASHAURI YA CHAMWINO YATAKIWA KUONGEZA BAJETI YA ELIMU
DODOMA: Halmashauri ya Chamwino imetakiwa kuongeza bajeti kwenye sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kutenga fedha na kuongeza idadi za shule jumuishi ili kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Akitoa mapendekezo ya jukwaa la Vijana Wilaya ya Chamwino,kuhusu maboresho katika sekta ya elimu,katika mkutano ulioandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Tanzania,Mjumbe wa Jukwaa hilo,Magreth Malongo amesema ili kufikia lengo namba 4 la maendeleo endelevu ya dunia,pamoja na kutatua changamoto zilizopo nguvu inahitajika katika ngazi ya Wilaya.
Amesema kuna haja ya Halmashauri hiyo kuongeza bajeti katika sekta ya elimu hasa katika madawati,nyumba za walimu na matundu ya vyoo kwani hali imekuwa sio nzuri katika Halmashauri hiyo yenye Majimbo mawili ya Mvumi na Chamwino.
“Sisi kama wanajamii tunapendekeza changamoto hizi zitatuliwe kupitia Mfuko wa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya na kuondoa msongamano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa,’’amesema Malogo.
Kwa upande wake,Mwakilishi wa Jukwaa hilo,Mariam Mahajile alisema kutokana na kuongezeka idadi wa watoto wenye mahitaji Maalum kuandikishwa kutoka watoto 35 mwaka 2015 hadi 61 mwaka 2021 walioko nje ya mfumo jukwaa hilo lilipendekeza Halmashauri kutenga na kuongeza idadi za shule jumuishi ili kuwasaidia.
‘’Kutenga Bajeti kwaajili ya watu wenye mahitaji maalum pamoja na kuongeza idadi ya walimu waliobobea kwenye taaluma hiyo kwani wanahitaji huduma za kutosha tofauti na wa kawaida,’’amesema Mahajile
Akipokea mapendekezo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Edson Sweti alisema wameyapokea mapendekezo hayo na kuahidi wataongeza bajeti hiyo huku akitoa maagizo kwa Maafisa Elimu kubaini walimu Maalumu ili waweze kwenda kwenye shule lengwa ili kupunguza uhaba huo.
‘’ Tunawalimu wa kutosha ambao tayari tushawapeleka kwa miaka mitano masomoni tuwapeleke kwenye shule lengwa ili wakafanye kazi lengwa , maana mwaka jana katika mapato yetu tulikusudia kukusanya bilioni 2.1 mpaka sasa tumekusanya kwa asilimia 92 mwaka unaokuja tumeongeza kutoka bilioni 2.1 mpaka bilioni 3,’’amesema Sweti.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya hiyo,Neema Milumbi amesema mapendekezo hayo yatawasaidia katika kusimamia, kufuatilia na kupanga bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.
‘’Wamezungumzia juu ya miradi ya jimbo , bajeti ni ndogo kama Milioni 98 au 99 lakini bajeti hiyo inagawanyika kwa majimbo mawili Mvumi na Chamwino bajeti hiyo ni finyu sana,”amesema na kuongeza
“Kwahiyo ni vigumu sana kama walivyoshauri iende kwenye tarafa moja kwa sababu fedha zile zipo kwaajili ya kuchochea miradi ya maendeleo.’’amesema kaimu Afisa elimu huyo.