- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAMEVULIWA UWANACHAMA CHADEMA
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzani nchini Chadema, Freeman Mbowe amesema wanachama 19 akiwemo Mwenyekiti wa Bawacha Taifa Halima Mdee wamevuliwa uanachama wa chama hicho kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kutoa baraka zake.
Mbowe ambaye alikuwa Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni ametoa tamko hilo leo usiku wa Ijumaa Novemba 27, 2020 majira ya saa 5 usiku wakati akisoma maazimio ya kikao cha kamati kuu kilichoketi kuanzia saa 3 asubuhi kuwajadili wabunge hao.
Wanachama hao Waliovuliwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Mbowe alizitaja hatua tatu ambazo kamati kuu imezichukua kabla ya kutangaza uwamuzi wa kuwavua uwanachama ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa miongoni mwao waliokuwa viongozi wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) na lile la wanawake (Bawacha) na kuagiza mchakato wa kujaza nafasi zao uanze mara moja.
“Tumeagiza kurugenzi yetu ya kisheria itafute taratibu mbalimbali za kisheria kupinga mchakato wa kuwapata wabunge 19 wa Chadema kwa sababu mchakato huo ni batili kuanzia hatua ya mwanzo maana wameghushi majina na waliopelekewa majina nao wameyapokea,” alisema Mbowe.
Mbowe amesema licha ya kuwaita kuhojiwa hawakutokea huku wakitoa sababu zinazofanana kwamba waongezewe siku saba wajitafakari kwa madai wanahofia usalama wao kwa madai kuwa kuna wanachama walijipanga kuwafanyia vurugu.
Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema wana nafasi ya kuomba radhi ili kurejeshewa uanachama wao na kama hawakuridhika na uamuzi huo wana haki ya kukata rufaa.
“Kikao cha kamati kuu hakikufanyika makao makuu ya chama tulikifanya katika hoteli ya Ledger Plaza (zamani Bahari Beach) Ili kuhakikisha wanakuwa huru zaidi ila wao hawakuja wote na pia tuliwapigia simu kusisitiza waje, hawa dada zetu wamekumbwa na nini,” amesema Mbowe.