- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALIMA MDEE MAHAKAMA YAMKUTA NA KESI YA KUJIBU
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Mbunge wa Kawe, Halima Mdee anayekabiliwa na kesi ya uchochezi kwa kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya Rais John Magufuli anayo kesi ya kujibu.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa uamuzi huo jana Mei 28, 2010 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Februari 20, mwaka huu upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao kufuatia mashahidi watatu waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi ambao leo mshtakiwa Mdee ameonekana na kesi ya kujibu.
Hata hivyo Mdee kupitia wakili wake Hekima Mwasipo amesema mteja wake atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi watano.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana