- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HALI YA MAANDAMANO NCHINI MAREKANI IMEPAMBA MOTO
Waandamanaji wanaopinga ubaguzi kwa mara nyingine tena wameingia mitaani jana jumapili katika miji tofauti tofauti nchini Marekani, kupaza sauti zao juu ya hasira dhidi ya ukatili wa polisi walioufanya dhidi ya Mmarekani mweusi George Floyd.
Wakati huo huo utawala wa rais Donald Trump uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika katika usiku wa siku tano kuwa ni magaidi wa ndani.
Wakati viongozi wa maeneo mbali mbali wakitoa wito kwa raia kuonesha hasira zao kwa njia ya uadilifu kuhusiana na kifo cha mtu mmoja mweusi ambaye hakuwa na silaha, amri ya kutotembea usiku iliwekwa katika miji kama Los Angeles, Houston na Minneapolis , ambayo imekuwa kitovu cha machafuko.
Maandamano yaliyokuwa yakiangaliwa kwa karibu zaidi yalitokea nje ya ofisi za serikali katika mji pacha wa Minneapolis wa St.Paul ambako maelfu kadhaa ya waandamanaji walijikusanya kabla ya kuandamana katika barabara kuu.
"Tuna watoto wa kiume weusi, tuna ndugu weusi , hatutaki wafe. Tumechoka kuona hili likitokea, kizazi hiki hakina hilo, tumechoka kukandamizwa," alisema Muna Abdi, mwanamke mweusi mwenye umri wa miaka 31 ambaye alijiunga na maandamano.
Mamia ya polisi na vikosi vya ulinzi wa taifa viliwekwa kabla ya maandamano licha ya kuwa hakukuwa na ripti za ghasia.
Wakati hakuna hali iliyojirejea la ghasia za kiwango kikubwa ambacho kilitikisa miji katika siku za hivi karibuni, waporaji walivamia maduka na maeneo mbali mbali katika mji wa Philadelphia.