- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: GWAJIMA ATAKA MASHEIKH WA UAMSHO KUACHILIWA HURU
Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe (CCM), Askofu Josephat ameiomba Serekali kushughulikia mapema iwezekanavyo suala la masheikh 23 wa Uamsho na wengine 64 waliopo mahabusu mkoani Arusha, Gwajima amsema ni bora wahukumiwe kuliko kuendelea kukaa mahabusu bila kujua hatima yao.
Akizungumza bungeni leo Ijumaa Aprili 23, 2021 katika mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2021/22, Askofu Gwajima amesema masheikh wa Uamsho wana zaidi ya miaka tisa mahabusu, kuhoji itakuwaje kama wakifikisha miaka 20 bado wapo mahabusu na ikabainika kuwa hawana hatia.
Huku akigusia sheria alizodai kuwa zina dosari, kiongozi huyo wa kiroho amesema, “naiomba Serikali kuziangatia upya sheria hizi; sheria ya utakatishaji fedha, sheria ya uhujumu uchumi pamoja na sheria ya ugaidi.”
Gwajima amesema kuna Watanzania wengi wapo mahabusu kwa sababu ya kubambikiziwa makosa ya utakatishaji fedha na watu wasio waaminifu.
“Bunge hili wakati linapitisha sheria hizi na kufikia mahali kwamba hakuna dhamana kabisa. Nia ya Bunge ilikuwa ni nzuri lakini utekelezaji wake umeingia dosari kubwa,” amesema.
Akitoa mfano wa watu wanaokwenda kwa wafanyabiashara kudai mapato au malimbikizo ya mapato kwamba wanakuwa hati za mashitaka kwamba asipopewa kiasi fulani cha fedha anampa kesi ya uhujumu uchumi au utakatishaji fedha.
Gwajima amesema kwa takwimu alizopata hadi sasa kuna watu 1,701 waliopo mahabusu kwa sababu ya utakatishaji fedha au uhujumu uchumi.
“Kwa kuwa kazi mojawapo ya Bunge ni kutunga sheria na kufuta sheria, haileti maana hadi leo wale masheikh wa Uamsho 23 wa Zanzibar wapo mahabusu hadi leo. Leo ni miaka tisa.”
“Lakini haitoshi, kuna masheikh 64 huko mkoani Arusha ambao wako mahabusu kwa sababu ya sheria ya ugaidi ambayo haina dhamana. Mimi sielewi kwa nini masheikh tu ndiyo magaidi kwani hakuna watu wengine ambao ni magaidi,” amehoji.