- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: GWAJIMA AGOMEA KITI NA MIC YA KAMATI YA BUNGE
Dodoma. Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima, amekataa katu katu kukaa kwenye kiti pamoja na kutumia kipaza sauti alichokuwa ameandaliwa alipofika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mwenyekiti wake Emmanuel Adamson Mwakasaka, na kuomba vibadilishwe.
Haijafahamika sababu hasa za Mbunge huyo kuomba abadilishiwe vitu hivyo. Lakini Kamati ya Bunge ilibadilisha vitu hivyo mara baada ya Gwajima kutoa masharti hayo.
Gwajima, amechukua hatua hiyo alivyowasili kwenye viwanja vya Bunge hii leo kwa ajili ya kuhojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili, ambapo aliomba kubadilishiwa vitu hivyo.
Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima aliwasili kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma hii leo majira ya saa 6:40 mchana kwa ajili ya kuhojiwa ikiwa ni kuitikia wito wa Spika wa Bunge Job Ndugai alioutoa Agosti 21 mwaka huu, ambapo pia kabla ya mahojiano aliomba pia msaidizi wake amletee dawa zake anywe.
Askofu Gwajima alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 4 (1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya kanuni za kudumu za Bunge toleo la Juni 2020 ambayo inaipa mamlaka kamati hiyo kuchunguza mambo yanayohusu maadili ya wabunge yanayopelekwa kwa Spika.