Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:43 pm

NEWS: GUTERRES AMTAHADHARISHA HAFTAR ,HAKUNA MAZUNGUZO YA KIJESHI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amemwambia kamanda wa vikosi vya mashariki mwa Libya, Khalifa Haftar, kuwa hakutakuwa na suluhisho la kutumia jeshi katika mzozo wa Libya na badala yake kutakuwa na suluhisho la Kisiasa la kufanya majadiliano ya pande mbili.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema Kamanda Haftar alimpigia simu Guterres Jumatano na walijadili maendeleo ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta. Mwezi uliopita, wanajeshi wa Haftar walilazimika kurudi nyuma kutoka mji mkuu Tripoli ilipo serikali ya umoja wa kitaifa, GNA.

Kulingana na Dujarric, katibu mkuu huyo amemwambia Haftar kwamba suluhisho linaweza tu kuwa la kisiasa, ambalo litasimamiwa na Walibya wenyewe. Guterres pia amesisitiza pendekezo la Umoja wa Mataifa, la kutaka kufanyike mazungumzo kati ya pande hizo mbili kupitia Tume ya Pamoja ya Kijeshi ya Libya.

Aidha msemaji huyo ameeleza mshtuko wa Guterres baada ya kugunduliwa makaburi ya watu wengi katika maeneo yaliyopokonywa vikosi vya Haftar hivi karibuni. Guterres amesisitiza haja ya kuheshimiwa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu pamoja na sheria ya kimataifa ya ubinadamu