Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 2:10 pm

NEWS: GUTERRES AMEUTAKA UCHAGUZI WA TANZANIA KUWA HURU NA HAKI

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ametaka mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kuwa huru na haki ili kuwapa fursa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema kuwa Guterres amewataka viongozi wote wa kisiasa na wafuasi wao kushiriki shughuli ya uchaguzi kwa amani na kujiepusha na vurugu.

Ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama ambayo yataruhusu Watanzania kutumia haki yao ya kiraia ya kupiga kura.

Amesisitiza juu ya UN kuunga mkono juhudi za Tanzania katika kuhakikisha kunakuwa na maendeleo endelevu na kujenga mustakabali mzuri.

"Wakati Watanzania wanajiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28, natoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa upigaji kura unafanyika kwa umoja na kwa amani," amesema Guterress.