Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 2:35 pm

NEWS: FIFA YAMFUGIA RAIS WA MPIRA WA MIGUU AFRIKA

Shikisho la soka duniani FIFA limemfungia Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na madai ya rushwa,.

Taarifa hiyo ya FIFA imetolewa hii leo Jumatatu (Novemba 23, 2020).

Rais Ahmad, anayetokea nchini Madagascar, amekuwa rais wa CAF tangu Machi 2017 na alikuwa anawania tena nafasi hiyo kabla ya Fifa kumzuia kushiriki "katika masuala ya uongozi".

Katika taarifa yake, Fifa imesema Ahmad alikiuka jukumu lake la utii, kutoa zawadi na upendeleo mwingine, ubadhirifu wa fedha na kutumia vibaya nafasi yake kama rais wa CAF.

Ahmad pia amepigwa faini ya dola 220,000 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh450 milioni za Kitanzania) na Fifa kwa vitendo hivyo, ambavyo vinahusiana na "kuandaa na kugharimia mahujaji wa Umrah kwenda Makka" na kuhusika kwake katika kwake katika mkataba wa CAF na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo.