- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DR. MPANGA ATOA MAAGIZO HAYA KWA WIZARA MBILI
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia SIDO kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Balozi za Tanzania nje ya nchi katika kupata teknolojia rafiki, mitaji, kutafuta masoko ili kuendeleza viwanda vidogo na vya kati hapa nchini, kukuza ajira na kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi.
Dkt. Mpango ameyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya tatu (3) ya SIDO Kitaifa yanayolenga kutoa fursa kwa wajasiriamali kupanua wigo wa masoko ya bidhaa, kuongeza uzalishaji, kubadilishana uzoefu na ujuzi na kuboresha bidhaa kulingana na mahitaji ya soko ambayo yameanza tarehe 21 hadi 31 Septemba 2021 katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Akizungumzia Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ya SIDO ya mwaka huu inayosema “Pamoja Tujenge Viwanda kwa Uchumi na Ajira Endelevu”, Dkt. Mpango ameagiza kuwa maonesho au maadhimisho mbalimbali yanayofanyika nchini yafanyiwe tathmini ya utekelezaji wa Kauli mbiu husika ya kipindi/mwaka uliotangulia.
Aidha, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kufanya tathimini kuhusu utekelezaji wa malengo ya kuanzishwa kwa SIDO pamoja na kupitia mahitaji ya bajeti yake na kutoa mapendekezo ya mikakati mipya ya kuiboresha na kuitafutia vyanzo vingine vya mapato ili kuiwezesha Tanzania kukidhi mahitaji ya uchumi wa kati.
Vile vile, ameelekeza SIDO na Taasisi zote za umma na binafsi zinazojihusisha na maendeleo na teknolojia ya viwandani zichukue hatua za dhati na kujiwekea malengo ya kulinyanyua Taifa katika utengenezaji wa mashine mbalimbali za kuchakata na kuongeza thamani mazao ya kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi na nafuu.
Makamu wa Rais pia amezitaka Taasisi za kifedha kubuni na kutoa Mikopo kwa wajasiriamali wadogo yenye riba nafuu, kutoa elimu kuhusu ubora wa miradi, usimamizi wa miradi na matumizi adili ya mikopo inayotolewa ili kuongeza uzalishaji, ajira na kupunguza umaskini huku akiwataka wajasiriamali hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.