- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DKT. MPANGO KUZINDUA MPANGO WA MAKAZI 1000 KWA WATUMISHI WA UMMA.
DODOMA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajia kuzindua Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma utakaofanyika Desemba 11,2024 Jijini Dodoma.
Akizunguumza na waandishi wa habari leo Jumatano Desemba 4,2024 Ofisini kwake Jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa huo Rosemary Senyamule amesema "Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia taasisi yake ya Watumishi Housing Investments (WHI) imeandaa hafla muhimu ya Uzinduzi wasiku ya Jumatano tarehe 11 Disemba, 2024 katika eneo la Mradi wa Nyumba Njedengwa jijini Dodoma, "
Aidha, Amesema Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha ustawi wa watumishi wa umma, kuhakikisha wanapata makazi bora, yenye gharama nafuu, na salama.
"Kupitia mpango huu, watumishi wa umma wanapata fursa ya kumiliki nyumba kwa masharti nafuu, hatua inayolenga kuboresha hali ya maisha na kuongeza ufanisi kazini. Aidha mpango huu una lengo la kuwawezesha wananchi na hasa watumishi wa umma kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba, " Amesema Senyamule
Hata hivyo ameendelea kwa kusema Watumishi Housing Investments kupitia mpango huu imetoa mikopo yenye masharti nafuu kwa watumishi wa umma ili kuwawezesha kumiliki nyumba kwa urahisi zaidi.
" Utekelezaji wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma ni dhamira pana ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa ya kumiliki makazi bora," Ameongeza Senyamule.
Mbali na hayo Rc huyo ametoa wito kwa Wanadodoma na wananchi wote kwa ujumla Kubiak kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.
Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma ulianza kutekelezwa mwaka 2014 chini ya usimamizi wa Watumishi Housing Investments (WHI) na hadi sasa, zaidi ya nyumba 1,000 zimejengwa katika mikoa 19 nchini Tanzania, ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Simiyu Mtwara.