- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS; DKT. MPANGO ATOA MAAGIZO KWA WIZARA YA AFYA NA TAMISEMI
DODOMA: Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto zimetakiwa kuhakikisha zinaweka mfumo ambayo utasaidia misaada yote inayotolewa na wasamaria wema katika vituo vya kulea Watoto yatima na wasiojiweza inawafikia walengwa.
Hayo yamezungumza leo June 16,2021, jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dkt, Philip Mpango wakati akizindua makao ya taifa ya watoto, ambapo ametoa maagizo kwa Wizara hizo ikiwemo kuhakikisha zinaweka mfumo wa kuhakikisha misaada inayotolewa na wasamaria wema katika vituo vya kulea Watoto yatima na wasiojiweza inawafikia walengwa.
Pia, amezitaka kusimamia na kuhakikisha makao hayaanzishi kiholela bila kuwa na leseni,pamoja na kuhakikisha makao yanakuwa na walezi wa kutosha na wenye sifa stahiki na utoaji wa huduma unazingatia taratibu za kiafya.
Pia,wasimamie na kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa kwa kuzingatia mila,tamaduni na desturi za kitanzania.
Aidha,Makamu wa Rais amesema kuwa yapo pia baadhi ya makazi ya watoto ambayo yameanzishwa bila kufuata utaratibu.
Kutokana na hayo ameitaka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Tamisemi kusimamia na kuhakikisha kuwa huduma katika makao ya watoto zinazotolewa kwa kuzingatia kiwango,matakwa ya sheria na kanuni husika.
Pia amezitaka Wizara hizo kuweka maandalizi ya wototo kurejea katika jamii kama vile kuwachanganya na wenzao katika maeneo mbalimbali kama vile mashuleni,vyuo vya ufundi na kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii yanayohusu watoto.
Awali akimkaribisha,Makamu wa Rais, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Dkt ,Dorothy Gwajima amesema Juni 16 ni siku ya mtoto wa Afrika ambapo nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania wanaadhimisha siku hiyo.
Amebainisha kwamba kama sehemu ya maadhimisho hayo serikali imezindua Makao ya watoto ya Kikombo Mkoani Dodoma ambapo ameitaka jamii kufanya tathimini ni sababu ipi inayopelekea watoto wa mitaani kuongezeka.
Hata hivyo amesema Ujenzi wa Makao hayo unatarajia kuwezesha serikali kutatua changamoto za huduma katika Makao ya watoto kwani kituo cha Kurasini ni kidogo.
Hata hivyo ameeleza kuwa , Ujenzi wa Makao ya Taifa hayo ya watoto yamegharimu Jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 5.5 Sawa Shilingi bilioni 12.7 za kitanzania ambapo mpaka sasa makao Makuu hayo yanawatoto 28 ambao wanaume ni 16 na watoto wa kiume ni 12.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo amesena kuwa kuna tatizo kubwa sana la watoto wa mitaani waliokosa malezi bora hivyo anaamini kupitia kuwepo kwa kituo hicho kutaleta matokeo chanya.
"Tuna watoto mil.20 lakini mil. 3 wanaudumavu hivyo tunahaja yakutoa elimu kwa familia"amesema Nyongo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Antony Mavunde amesema inapofika majira ya jioni katika eneo la Nyerere Square watoto wengi hutandika mabox na kulala chini.
"Ujenzi wa kituo hichi naamini watanufaika maana wengine wanatumia gundi na madawa ya kulevya..