Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 12:55 pm

News: Dkt. John Pombe Magufuli ameitumia salamu za rambirambi familia ya Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi

DAR ES SALAAM; Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es slaaam Dkt. Didas Masaburi aliyefariki dunia jana tarehe 12 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea taarifa ya kifo cha Dkt. Didas Masaburi kwa mshituko na masikitiko makubwa na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.
"Poleni sana familia ya Dkt. Didas Masaburi, najua huu ni wakati mgumu sana kwenu, lakini niwahakikishie kuwa sote tumeguswa sana na msiba huu kwa kuwa tumempoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini" amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

Image result for Salamu za rambirambi za magufuli