- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DIAMOND AAHIDI KUMSOMESHA MWANAFUNZI MAREKANI AU UINGEREZA
Dar es Salaam: Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameahidi kumpa ufadhili mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari Rugambwa atakayefanya vizuri katika mtihani wake wa kidato cha nne utakaofanyika mwaka 2019.
Diamaond ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 19, 2019 wakati akitoa utambulisho kwa timu itakayoshiriki tamasha la Wasafi Festival wakati walipoitembelea shule hiyo iliyopo mkoani Kagera, nchini Tanzania.
Diamond amesisitiza kuwa ni yule atakayefaulu kwa kiwango cha juu katika mtihani huo.
Mkali huyo wa Kibao cha KANYAGA kilichoachiwa hivi karibuni amesema atazungumza na uongozi wa shule hiyo ili kupanga mikakati ya kufanikisha jambo hilo. Diamond amesema atazungumza na wadhamini wake katika tamasha la Wasafi ambao ni Global Education Link kwa ajili ya kupata nafasi moja ya ufadhili.
“Naamini hapa kila mtu ana kipaji tofauti na ili ufikie malengo lazima tusome kwa bidii katika masomo yetu, sasa kwa kuwa mmenifurahisha nitazungumza na walimu wa hapa.”
“Kwa mtu anayefanya vizuri katika masomo nitampa udhamini wa kwenda kusoma Uingereza au Marekani na hii kwa msaada wa chuo cha Global Education Link nitawaomba wanipatie nafasi ya mtu mmoja wa kwenda kusoma huko,” amesema Diamond.