Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:40 pm

NEWS: DC AWAONYA WANAUME WANAONYONYA MAZIWA YA WAKE ZAO

Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Siriel Mchembe amewaonya Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao ambao wapo kwenye hatua ya kuwanyonyesha Watoto wao, kuacha tabia hiyo mara moja kwasababu wanawafanya Watoto wao wasipate maziwa ya kutosha kwa ajili ya kuboresha afya zao.

DC Mchembe amesema tabia hiyo imejengeka kwa kuendekeza imani potofu kwamba mwanaume akinywa maziwa ya mama anaye nyonyesha atapata vitu fulani fulan(nguvu za Kiume).

DC Mchembe ametoa kauli hiyo baada ya Wanawake wanaonyonyesha Wilayani katika wilaya yake ya Handeni kumuomba awasaidie kupaza sauti na kukemea Wanaume wao kuacha tabia ya kuwanyonya maziwa kwa madai ya kwamba yanaongeza hizo nguvu za kiume.

Wanawake hao wametoa kauli hiyo kwa Mchembe kwenye maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika katika mji mdogo wa Mkata wilayani humo.

"Niwashauri Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao waache, wanatumia chakula cha Watoto na hiyo inasababisha mtoto kupata utapiamlo maana hawapati maziwa ya kutosha, hakikisheni mnashirikiana kwenye malezi haya mambo mengine acheni" amesema Mchembe

Ofisa lishe halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Julia Charo amesema kuwa hadi Juni 21, mwaka huu watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano waliobainika kuwa na uzito pungufu ni watoto 3,856 sawa na asilimia 14 ya watoto wote waliohudhuria kliniki.

Amesema kwa upande wa watoto waliopata udumavu ni asimilia 34 ya watoto wote waliopelekwa na kuhudumiwa katika kliniki na wajawazito 7519 waliopimwa wingi wa damu 102 walikutwa na upungufu mkali wa damu