- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: DAWA YA MKONGO YAPIGWA STOP
Dar es salaam. Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini Tanzania, limeipiga marufuku matumizi ya dawa aina ya Hensha maarufu Mkongo, inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam na kuifutia usajili dawa hiyo.
Akizungumza na wanahabari leo Jumatano Julai 27,2022 Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, mjini Morogoro amesema dawa hiyo inabidi iondoke sokoni mara moja
Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake, lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.
Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.
Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.