- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: CIA nchini Marekani wamesema Rais mteule Bwana Donald Trump alisaidiwa na UrusI kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita
Washington: Maafisa usalama nchini Marekani CIA wamepata RipotI inayo onyesha uwepo wa msaada ulio tumika kumsaidi Aliye kuwa mgombea wa chama cha Republican Bwana Donald Trump kushinda uchaguzi mkuu ulio fanyika hivi karibuni nchnini Marekani.
Ripoti moja katika gazeti la New York Times inasema kuwa vitengo hivyo vina uhakika wa kiwango cha juu kuhusu hatua hiyo ya Urusi ya udukuzi.
Ripoti nyengine ya maafisa hao iliotolewa na Gazeti la Washington Post pia ilitoa maoni kama hayo.
Lakini upande wa Bw Trump umepuuzilia mbali matokeo ya ripoti hiyo, ukisema hawa ni watu wale wale waliosema kuwa Sadaam Hussein anamiliki silaha za kuangamiza.
Maafisa wa Urusi kwa mra nyengine wamekana kuhusika na udukuzi wowote wa kumsaidia Trump katika uchaguzi huo.
Siku ya Alhamisi rais Obama alitaka uchunguzi kufanywa kufuatia misururu ya udukuzi wa mitandao inayodaiwa kutekelezwa na Urusi wakati wa uchaguzi.
Udukuzi huo ulilenga barua pepe za chama cha Democratic na mshauri wa mgombea wa urais Hillary Clinton.