- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: China yaonesha ubabe wake baada ya kuzindua ndege za kivita zenye nguvu zaidi Duniani
Beijing: China imeonesha hadharani ndege zake mpya za kivita aina ya J-20 ambazo zina uwezo wa kujificha kwenye anga zisionekane kwenye mitambo ya rada. hii imeifanya china kuonekan kama tishio kwenye ulimwengu wa teknologia ya kijeshi ulimwenguni.
Jana Ndege mbili za aina hiyo zilipaa angani kwa kwa dakika 1 wakati wa maonesho ya ndege ya Zhuhai katika mkoa wa Guangdong.
Maonesho hayo huwa makubwa zaidi nchini humo na huwakutanisha waundaji na wanunuzi wa ndege Duniani.
Ndege hizo zinatazamwa na wengi kama ishara ya hamu ya Beijing kuboresha na kuimarisha uwezo wake kijeshi.
Rais wa China Xi Jinping anataka kuimarisha majeshi ya nchi yake huku taifa hilo likiendelea kudhihirisha ubabe sana kuhusu umiliki wa maeneo ya bahari Kusini na Mashariki mwa China.
Ndege hizo za J-20 zimeundwa na kampuni ya Chengdu Aircraft Industries Group, ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la ndege la China ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Aviation Industry Corporation of China.
Baadhi wamelinganisha ndege hizo na ndege aina ya F-22 Raptor za Lockheed Martin.
Mchanganuzi wa masuala ya ndege Bradley Perret amesema ndege hiyo "bila shaka ni hatua kubwa katika uwezo wa kivita wa China".
Nahizi ni picha ya ndege zingine