- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: Chikota ataka Kuazishwa Mamlaka ya Maji ya Mji wa Nanyamba
BUNGENI DODOMA; Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota ameiomba Serikali kuanzisha Mamlaka ya Maji ya Mji wa Nanyamba kwakuwa halmashauri hiyo ina hadhi, imesajiliwa na sheria ya maji inaruhusu.
Ombi hilo alilitoa bungeni jana wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Chikota alisema halmshauri ya mji wa Nanyamba ina hadhi imesajiliwa kama halmashari ya mji na kwa mujibu wa sheria ya maji hivyo wana uwezo wa kuwa na mamlaka yao kwakuwa kwa sasa wanahudumia kwa dharura na Mtuwasa.
“Mheshimiwa Waziri tunaomba ulifanyie kazi tuwe na mamlaka yetu ya mji wa Nanyamba maana tuna vigezo vyote, badala ya kuendelea kuhudumia na Mtuwasa,”alisisitiza.
Aidha, suala la maji mkoani Mtwara hali ni tete na kwamba hata kwenye kikao kilichopita cha kamati ya ushauri cha mkoa ajenda hiyo iliwekwa maalum.
Alimpongeza Waziri mwenye dhamana Jumaa Aweso kwa kukutana na wabunge wa Mtwara na kuwasilikiza na kuanza kulifanyia kazi suala hilo.
Alifafanua kuwa walipeleka mambo mawili kwa serikali na kwamba yameshafanyiwa kazi likiwemo la mradi wa maji Makonde ulioondolewa kwenye miji 28 kurejeshwa kwakuwa unahudumia mkoa huo kwa asilimia 40, halmshauri nne ambazo ni Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba na Nanyamba.
“Kwahiyo mradi huu ukitekelezwa ipasavyo tutakuwa tumepunguza tatizo la maji katika mkoa wa Mtwara, na nakuomba usikilize ushauri wetu kwamba mradi wa Makonde kupitia chanzo cha mitema kina maji mengi sana utekelezwe,”alisema Mbunge Chikota.
Aliongeza katika ombi lingine la kuruhusu matumizi ya maji ya mto Ruvuma kwenda kwenye chanzo cha miembe chini jimboni humo unagusa vijiji 74, na kata 13 za eneo hilo zikiwemo Nanyamba, Mtwara Vijijini na inawezekana ukavutwa na kuingia jimbo la Mtama.
“Mradi huu ukitekelezwa utatatua changamoto nyingi maana mradi wa miembe chini nimesikia hapa kiasi cha sh. bilioni sita kimetengwa hivyo naomba fedha hizo zitolewe kwa wakati ili maji yawe ya uhakika na wawekezaji wakija wakute huduma zipo,”alisema.