- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHATANDA AKEMEA TABIA ZINAZOKWAMISHA WATOTO KUSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO
IRINGA: Mwenyekiti wa UWT Taifa *Ndg Mary Pius Chatanda (MCC) amewataka wazazi kuacha mara moja tabia ya kuozesha watoto wakiwa na umri mdogo au kuwasafirisha mikoani kwenda kufanya kazi za ndani.
Akizungumza na wananchi wa Igowole mkoa Iringa, Chatanda amesema;
"Rais Samia ametengeneza na kuboresha miundombinu mizuri ya shule, ameajiri walimu wa kutosha na kuongeza vifaa ikiwemo vitabu kwasababu anataka watoto wasome katika mazingira mazuri ili waweze kufaulu, waweze kuajirika na kuajiriwa na waweze kujitegemea kiuchumi. Mkiwaozesha watoto wadogo au kuwapeleka kufanya kazi za ndani, mnakosea sana"
Chatanda amepiga marufuku tabia hii kwani inawanyima watoto haki ya kupata elimu na inakwamisha jitihada za kuwainua kiuchumi Watanzania wote ususani watoto wakike zinazofanywa na Serikali ya CCM kupitia Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025.