Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:09 am

NEWS: CHAMA TAWALA NCHINI BURUNDI CHARUDI MADARAKANI.

Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ndio atakuwa Mrithi wa Rais Pierre Nkurunziza hii ni baada ya Tume ya Uchaguzi nchini humo kumtangaza kama mshindi jana kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho kimedaiwa kukumbwa na visa vya udanganyifu.

Ndayishimiye ametangazwa kushinda baada ya kupata asilimia 68.72 ya kura zilizopigwa. Tume ya uchaguzi nchini Burundi ambayo imetangaza matokeo hayo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini humo, imesema Agathon Rwasa wa chama cha National Freedom Council (CNL) ambaye ndiye mshindani mkuu wa Ndayishimiye amepata asilimia 24.19 ya kura.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, asilimia 87.7 ya wapiga kura waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo.

Hapo awali, msemaji wa Rwasa alisema kilichotokea kwenye uchaguzi huo ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung'ang'ania madaraka