Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:21 pm

NEWS: CHAMA CHA WAVUVI CHAIPA SIKU 4 SEREKALI KUONDOA TOZO

Mwanaza. Chama cha Wavuvi Tanzania (TAFU) Kanda ya Ziwa kimetoa siku nne kwa serikali ya Tanzania kupunguza tozo ya asilimia mbili ya mauzo ya samaki viwandani inayotozwa kwasasa ili angalau ifikie asilimia 0.5, pamoja na kuiomba serikali iwaondoe kwenye kodi ya makadirio ya mwaka kwa lengo la kuwapa nafuu wa kumudu gharama za uendeshaji wa shughuli zao.

Mwenyekiti wa chama hicho Bakari Kadabi amesema kuanzia Julai 14 mwaka huu, wavuvi wapatao 100 waliopo kanda ya ziwa watasitisha kupeleka samaki viwandani hadi hapo muafaka wa suala hilo utakapopatikana.

Kadabi amesema kuwa jiji la Mwanza pekee lina jumla ya viwanda 6 vya kuchakata minofu ya samaki kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi.

Kwa upande wao, baadhi ya wavuvi pamoja na mawakala wa uuzaji wa samaki viwandani wameiomba serikali ilifanyie kazi ombi lao la punguzo ya asilimia 2, huku wakisema wako tayari kuendelea kulipia ushuru wa halmashauri unaoanzia shilingi 100 hadi 300 kwa kilo ya samaki.

Mwanasheria wa Chama cha Wavuvi Tanzania Mayalu Kasile akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili tozo ya asilimia 2, pamoja na kuazimia kwenda kuonana ama na Waziri Mkuu au Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ili kufikisha kilio chao kwa nia ya kulinda mitaji yao.